Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 19:30

Viongozi wa EU wakubaliana kuipa msaada wa dola bilioni 50 Ukraine


 Charles Michel
Charles Michel

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kwa kauli moja wamekubaliana Alhamisi kuipa Ukraine msaada wa jumla ya dola za Marekani bilioni 50, na kumaliza upinzani ambao Hungary iliuleta huko nyuma. 

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisherehekea makubaliano hayo, akisema EU ilikuwa inaonyesha uongozi na uwajibikaji katika kuiunga mkono Ukraine na wanajua “nini kiko hatarini.”

“Hii iko imara, kwa muda mrefu, ufadhili unaotabirika kwa Ukraine,” Michel alisema kupitia X, mtandao uliokuwa zamani Twitter.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine alikaribisha kura hiyo ya pamoja, akisema “imethibitisha umoja imara wa EU.”

Msaada endelevu wa kifedha wa EU kwa Ukraine utaimarisha kwa muda mrefu uthabiti wa kiuchumi na kifedha, ambao bado ni muhimu kama ilivyo wa kijeshi na shinikizo la vikwazo dhidi ya Russia,” Zelenskyy alisema kupitia X.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema kupitishwa kwa msaada huo Alhamisi ni kinyume “na kauli zozote kuhusu madai kuwa ‘msaada umewachosha wafadhili au unapungua” kwa ajili ya Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG