Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:19

Nepal yaitaka Russia kuwarejesha raia wa Nepal wanaopigana Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal Narayan Prakash Saud akiongea na shirika la habari la Associated Press katika ofisi yake huko Kathmandu, Jan. 25, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal Narayan Prakash Saud akiongea na shirika la habari la Associated Press katika ofisi yake huko Kathmandu, Jan. 25, 2024.

Nepal imeitaka Russia kuwarejesha mamia ya raia wa Nepali ambao waliandikishwa kupigana dhidi ya Ukraine na pia miili ya wale waliokufa katika vita hiyo kurejeshwa nyumbani, mwanadiplomasia wa juu wa Nepal alisema Alhamisi.

Jeshi la Russia linakadiriwa kuwa liliwaandikisha zaidi ya raia wa Nepali 200 kupigana huko Ukraine na angalau 14 kati yao wamefariki huko, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepali Prakash Saud alisema katika mahojiano na shirika la habari la AP.

Tumewataka Russia kusitisha kusajili mara moja raia wa Nepali, na mara moja kuwarejesha wale ambao tayari wanatumikia jeshi hilo, kurejesha miili ya wale waliouawa, na kuwatibu na kuwarejesha nyumbani wale waliojeruhiwa katika mapigano,” Saud alisema.

Nepal pia inataka fidia ya fedha kutoka Russia kwa ajili ya familia za raia wa Nepali ambao waliuawa katika mapigano, Suad alisema.

Kati ya wale raia wa Nepali 14 waliothibitishwa kuuwawa, Russia ilisema inayo miili 12. Watu wengi wa Nepali wanataka miili ya ndugu zao waliofariki ichomwe kulingana na taratibu za kidini.

“Tuna taarifa kuwa raia wetu watano waliokuwa wakipigana kwa niaba ya Warrusia wametekwa na upande wa Ukraine. Tunautaka upande wa Russia kufanya juhudi zote ili kuwezesha kuachiliwa,” alisema Saud.

Maafisa wa Russia hawajatoa tamko lolote kuhusu usajili wa mataifa ya nje kuingizwa katika huduma za kijeshi huko Ukraine, lakini ripoti za vyombo vya habari zimesema licha ya waliosajiliwa kutoka Nepal jeshi la Russia limewasajili baadhi ya watu kutoka Cuba.

Sheria ya Russia inaruhusu raia wa kigeni kusajiliwa katika jeshi lake baada ya kusaini mkataba na Wizara ya Ulinzi.

Mwezi Septemba, mamlaka nchini Cuba iliwakamata watu 17 kuhusiana na kile walichosema ni mtandao wa kusajili raia wa Cuba kwenda kujiunga na jeshi la Russia katika vita vyake huko Ukraine.

Mapema mwezi huu, Rais wa Russia Vladimir Putin alisaini amri ya kiutendaji kuharakisha mchakato wa kuwapatia uraia wa Russia wageni wanaojiandikisha katika jeshi la nchi hiyo huku Moscow ikijaribu kuongeza wanajeshi wake kwa taratibu mbalimbali, ikiwemo kuandikisha wahamiaji.

Ukraine pia inaaminika kuwa imeajiri baadhi ya raia wa Nepal kupigana kama wanajeshi, lakini Saud alisema hana taarifa zaidi kuhusu hilo.

Serikali ya Nepal imepiga marufuku raia wake kusafiri kwenda Russia au Ukraine kwa ajili ya kutafuta ajira, akisema wengi wao wamesajiliwa na jeshi la Russia kupigana katika vita vya Ukraine.

Saud alikutana na maafisa wa Russia pembeni ya mkutano wa Nchi Zisizo Fungamana na Upande Wowote (NAM) uliofanyika Uganda mapema mwezi huu na kujadili masuala hayo yote pamoja nao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG