Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:23

Mapambano yazuka katika Mkoa wa Russia kufuatia kifungo cha mwanaharakati


Polisi wa kutuliza ghasia wakiwasambaza wafuasi wa Fail Alsynov huko Baymak katika mkoa wa Bashkortostan, Russia, Jan. 17, 2024 video.
Polisi wa kutuliza ghasia wakiwasambaza wafuasi wa Fail Alsynov huko Baymak katika mkoa wa Bashkortostan, Russia, Jan. 17, 2024 video.

Polisi wa kutuliza ghasia wametumia gesi  ya kutoa machozi na kuwapiga waandamanaji kwa virungu katika jamhuri ya Russia ya Bashkortostan Jumatano baada ya kiongozi wa harakati za haki za binadamu kuhumiwa kifungo cha miaka minne.

Mapambano yalizuka kati ya polisi na umati mkubwa wa watu ambao walikusanyika kumuunga mkono mwanaharakati, Fail Alsynov.

Katika kesi ambayo vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia mahakamani, mahakama ilimkuta na hatia mwanaharakati kwa kuchochea chuki ya kikabila, dai ambalo alilikanusha.

Kanda za video zilizobandikwa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonyesha watu wakipiga kelele “Gesi!” na kukimbia.

Video moja ilionyesha mstari wa polisi wakiwapiga watu virungu.

Na nyingine ilionyesha mwanamke mmoja akiwasihi polisi waache kumpiga mtu mmoja aliyekuwa amelala ardhini.

Maandamano makubwa nchini Russia ni nadra sana kutokea kwa sababu ya hatari ya kukamatwa katika mikusanyiko yoyote ambayo mamlaka itayaona hayajaidhinishwa.

Maelfu ya watu wametiwa ndani katika miaka miwili iliyopita kwa kupinga vita nchini Ukraine,

Kipindi hiki ni nyeti kwa mamlaka, wakati wa kuanza kampeni za uchaguzi ambapo Rais Vladimir Putin anawania awamu mpya ya kipindi cha miaka sita.

Wakati ushindi wa Putin hauna mashaka, wachambuzi walisema kutakuwa na shinikizo kwa kiongozi wa mkoa wa Bashkortostan, Radiy Khabirov, kudhibiti hali ya huko ili kuepusha fedheha kwa Kremlin.

Alsynov alishutumiwa kwa kuwatukana wafanyakazi wahamiaji katika hotuba aliyoitoa Aprili 2023 katika maandamano ya kupinga mipango ya kuchimba dhahabu huko Bashkortostan, ambayo iko upande wa kusini wa milima ya Ural, Russia karibu na mpaka kati ya Ulaya na Asia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG