Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:47

Meya aliyefungwa jela Russia ajiunga kwenye vita vya Ukraine


Makazi ya watu binafsi iliyoharibiwa na kutokana na mashambulizi ya Russia karibu na mji wa Kryvyi Rih, Ukraine
Makazi ya watu binafsi iliyoharibiwa na kutokana na mashambulizi ya Russia karibu na mji wa Kryvyi Rih, Ukraine

Gazeti la Kommersant la Russia limesema Jumapili kwamba wakili wa aliyekuwa wakati mmoja Meya wa mji wa Russia wa Vladivostok, amejiandikisha kuingia kwenye vita vya Ukraine.

Kiongozi huyo sassa ameelekea kwenye uwanja wa vita, kufuatia kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi. Oleg Gumenyuk alipewa kifungo hicho mwaka uliopita kwa tuhuma za kupokea hongo la dola 432,000, wakati akiwa Meya wa mji huo kuanzia 2018 hadi 2021.

Baadaye alijiuzulu kufuatia shutuma nying dhidi ya utawala wake kutoka maafisa wa mji, na wale wa serikali kuu ya Russia. Gazeti hilo la Kommersant limenukuu wakili wake Andrei Kitaev, akisema kuwa amri iliyotolewa kwa Gumenyuk ilimhitaji kuripoti kwenye kituo cha kijeshi Desemba 22.

Maelfu ya wafungwa wa Russia wamejitolea kujiunga kwenye vita vya Ukraine, kwa matumaini ya kuachiliwa huru baada ya mapigano, kupitia msamaha uliotolewa na serikali, kwa wale amabao wangehudumu.

Forum

XS
SM
MD
LG