Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 07:18

Navalny ahoji kanuni za gerezani wakati kesi ikisikilizwa mahakamani


FILE PHOTO: Alexei Navalny
FILE PHOTO: Alexei Navalny

Kiongozi wa upinzani nchini Russia aliye gerezani Alexei Navalny alionekana mbele ya jaji wa mahakama ya juu  kwa njia ya video kuwasilisha ombi kudai haki ya muda mrefu zaidi wakati wa chakula na fursa ya kupata vitabu zaidi akiwa gerezani.

Akiwa amevaa sare nyeusi ya gerezani na amesimama nyuma ya vyuma, akiwa miguu chini, Navalny mwenye umri wa miaka 47, alionekana akiongea pole pole lakini alizungumza kwa mifano na kwa kirefu na bila ya kusoma popote.

Ilikuwa ni siku ya pili ambapo alikuwepo katika usikilizaji wa kisheria kwenye gereza la Arctic “Polar Wolf”, moja ya magereza yenye ulinzi mkali sana ambako alihamishiwa mwezi uliopita baada ya kupewa adhabu kadhaa za kifungo cha zaidi ya miaka 30.

Navalny alisema kanuni za magereza zinawapa fursa wafungwa ya kuwa na kitabu kimoja, kwahiyo mfungwa anapoamua kuchukua Biblia au Koran basi hawezi kupewa vitabu vingine vya dini au vyoyote vile, ikiwa ni pamoja na magazeti na majarida..

“Kitabu kimoja hakinitoshi. Ni dhahiri mnakiuka haki yangu ya dini,” amesema.

Pia alida kwamba muda wa chakula anaopewa ni mdogo mno.

Hoja zake zimechochea na majadiliano ya kina na jaji na mwakilishi kutoka wizara ya sheria kuhusu maktaba kwenye gereza, mipango ya muda wa kula na fanicha katika chumba chake.

Navalny mara kwa mara alitumia muda kama huo katika siku zilizopita kama njia ya kuikaidi mamlaka, akionyesha uthabiti wake katika kuhakikisha ana mahusiano na dunia ya nje licha ya masharti makali kwa kufungwa kwake.

Yeye na wafusi wake wanasema mashtaka mengi dhidi yake, kuanzia ubadhirifu mpaka msimamo mkali, yalifunguliwa ili kumnyamazisha kwa kumkosoa Rais Vladimir Putin.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG