Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 14:33

Rashia yawaweka kizuizini zaidi ya watu 5,000 kwa kuandamana dhidi ya vita huko Ukraine.


Polisi wamkamata muandamanaji mjini St Petersburg, katika maandamano ya kupinga uvamizi wa Rashia dhidi ya Ukraine. Februari 26, 2022. Picha ya AP
Polisi wamkamata muandamanaji mjini St Petersburg, katika maandamano ya kupinga uvamizi wa Rashia dhidi ya Ukraine. Februari 26, 2022. Picha ya AP

Rashia imewaweka kizuizini zaidi ya watu 5,000 Jumapili waliokuwa katika maandamano ya kupinga mashambulizi yaliyoamrishwa na rais Valdimir Putin dhidi ya Ukraine.

Maandamano hayo yalifanyika katika darzeni ya miji.

Ni idadi kubwa ya watu waliokamatwa kwa siku moja, kubwa zaidi kuliko watu waliokamatwa wakati wa msururu wa maandamano yaliofanyika mwaka uliopita wakati mpinzani mkuu wa serikali ya Moscow Alexei Navaly alipofungwa jela.

Navalny aliwaomba wanainchi wa Rashia kuandamana dhidi ya vita katika wito aliotoa akiwa gerezani.

Waandamanaji wanakabiliwa na kifungo cha jela kwa kuingia barabarani kuandamana.

Kundi linalofuatilia kukamatwa watu wakati wa maandamano OVD info, limesema zaidi ya watu 2,390 walikamatwa mjini Moscow pekee yake, kati ya 5016 waliyokamatwa katika miji 60 nchini humo .

XS
SM
MD
LG