Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:35

Russia yaona silaha za nyuklia muhimu kwa kujihami kufuatia hasara kubwa Ukraine - Ripoti


Picha ya mtandao wa Telegram ya Disemba 26, 2023ikionyesha moshi mkubwa kutoka katika meli ya kivita ya Russia kufuatia shambulizi la Ukraine kwenye bandari ya Feodosiyne, iliyoko chini ya mamlaka Russian huko Crimea.
Picha ya mtandao wa Telegram ya Disemba 26, 2023ikionyesha moshi mkubwa kutoka katika meli ya kivita ya Russia kufuatia shambulizi la Ukraine kwenye bandari ya Feodosiyne, iliyoko chini ya mamlaka Russian huko Crimea.

Hasara kubwa iliyopata Russia katika uvamizi kamili kwa Ukraine inamaanisha kuwa Moscow hivi sasa inaona matumizi ya silaha za nyuklia kuwa ni muhimu zaidi katika kuizuia na kuishinda NATO, kulingana na ripoti mpya kutoka taasisi ya kimataifa ya Masual ya Kimkakati (IISS).

Taasisi hiyo imeonya kuwa nchi za Magharibi lazima zichukue tahadhari zaidi dhidi ya tishio la shambulizi la nyuklia linaloongezeka.

Mwezi Februari 24, 2022, wakati vifaru vya kwanza vilipoingia mpakani mwa Ukraine wakati wakianza uvamizi huo, Rais wa Russia Vladimir Putin alitoa hotuba kupitia televisheni akiuonya ulimwengu “kuhusu matokeo mabaya ambayo hayajawahi kuonekana katika historia” iwapo yeyote atajaribu kuizuia Russia, tishio linaloonekana zaidi kuwa ni tishio la nguvu za silaha za nyuklia zitakazo tumiwa na Kremlin.

Ripoti ya IISS inasema hofu ya kuongezeka mvutano na Russia imesababisha nchi za Magharibi kusita kutoa silaha kuipa Kyiv.

Lakini kwa takriban miaka miwili sasa, ripoti ya kijasusi ya Marekani mwezi uliopita ilikadiria Russia imepoteza takriban wanajeshi 315,000 huko Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi huo, karibu asilimia 90 yao wakiwa ni wanajeshi wa awali – wingi wa vifo hivyo vikisababishwa na silaha zilizotolewa msaada na nchi za Magharibi.

“Russia imepoteza uthabiti hivi sasa katika uwezo wa kivita kwa sababu ya kila kitu walichopoteza katika vita vya Ukraine,” alisema William Alberque, mwandishi wa ripoti hiyo na Mkurugenzi wa Mkakati, Teknolojia na Udhibiti wa Silaha katika taasisi ya IISS.

Hiyo ina maana kuwa silaha za masafa mafupi za atomiki za Moscow, zinazojulikana kama Non-Strategic Nuclear Weapons au NSNW – zilizoundwa kwa ajili ya kutumika vitani – zimeanza kuwa muhimu zaidi kwa Kremlin, kulingana na Alberque.

“Kimsingi Russia ina makombora ya masafa mafupi na masafa ya kati, ya anga na ardhini na makombora yanayotumika kurushiwa baharini yenye uwezo wa kufikisha silaha za nyuklia katika eneo lote la vita na kuweza kuziweka nchi zote za NATO hatarini. NATO haina uwezo wa kukabiliana na nguvu hizo za nyuklia ambazo Russia inazo.”

Ripoti ya mwandishi wa VOA Henry Ridgwell.

Forum

XS
SM
MD
LG