Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 23:00

Russia yarejea kushiriki katika makubaliano ya usafirishaji nafaka za Ukraine


Meli iliyobeba nafaka kutoka Ukraine ikiwa imewasili Istanbul, Uturuki, Oct. 11, 2022.
Meli iliyobeba nafaka kutoka Ukraine ikiwa imewasili Istanbul, Uturuki, Oct. 11, 2022.

Russia imesema Jumatano inarejea kushiriki katika mkataba ulifikiwa kurahisisha usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia Black Sea.

“Muungano wa Russia unafikiria kuwa dhamana iliyopokelewa hivi sasa inatosheleza, na inaanza utekelezaji wa mkataba huo,” wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa yake.

Russia ilikuwa imesitisha ushiriki wake Jumamosi baada ya kudai kuwa Ukraine ilitumia ndege zisizokuwa na rubani kushambulia meli za Russia katika bahari ya Black Sea.

Umoja wa Mataifa na Uturuki zilisimamia mkataba kati ya Russia na Ukraine ili kuanza tena usafirishaji wa nafaka za Ukraine na kuruhusu meli za Russia kusafirisha mbolea mwezi Julai katikati ya mgogoro wa kimataifa wa chakula.

Usitishaji wa Russia ulivuruga usafirishaji katika siku za karibuni, wakati pande nyingine husika katika shughuli hiyo walijitahidi kusafirisha baadhi ya bidhaa kutoka bandari za Ukraine na kutekeleza ukaguzi kadhaa huko Istanbul kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Volodymyr Zelenskyy
Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila usiku, Jumanne kuwa njia ya upitishaji nafaka hizo “inahitaji kuwa ya kuaminika na yenye ulinzi wa muda mrefu.”

“Russia ni lazima ifahamu wazi kuwa itakabiliwa na majibu makali kutoka ulimwenguni kwa hatua yoyote itakayo vuruga usafirishaji wetu wa chakula,” Zelenskyy alisema. “Hii ni suala la uhai wa mamilioni ya watu.”

Silaha za Iran

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Jumanne pia ilieleza “wasiwasi” kuwa Russia inaweza kujaribu kupata silaha zaidi kutoka Iran ili kuzitumia katika vita yake dhidi ya Ukraine.

Hivi karibuni Russia ililenga miundombinu ya kiraia ikitumia droni zilizotengenezwa na Iran, na wafanyakazi wa Iran wanalisaidia jeshi la Russia kufanya mashambulizi kwa kutumia droni kutoka Rasi ya Crimea, kulingana na Marekani.

FILE - Droni za Iran zikiwa zinaandaliwa kufanyiwa majaribio, kama zilivyoripotiwa na jeshi la Iran, August 24, 2022.
FILE - Droni za Iran zikiwa zinaandaliwa kufanyiwa majaribio, kama zilivyoripotiwa na jeshi la Iran, August 24, 2022.

“Tunao wasiwasi kwamba Russia inaweza kutafuta silaha za uwezo mkubwa zaidi kutoka Iran, kwa mfano, makombora ya ardhini kwa ardhini, kuyatumia nchini Ukraine,” Ryder alisema.

Kituo cha televisheni cha CNN chenye makao yake Atlanta, kimeripoti kuwa Iran inajiandaa kupeleka takriban silaha 1,000 zaidi, ikwemo makombora ya ardhini kwa ardhini, na makombora ya balistiki ya masafa mafupi na ndege zaidi zisizo na rubani na za kujitoa muhanga.

Mwandishi wa VOA Pentagon Carla Babb amechangia katika habari hii.

XS
SM
MD
LG