Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 11:06

Ukraine kunasa makombora, Putin kukutana na Erdogan, Poland inakagua maficho dhidi ya mabomu


Ndege za kivita za Russia aina ya Mig-31
Ndege za kivita za Russia aina ya Mig-31

Ujerumani imeahidi kutoa msaada wa mitambo ya kisasa kwa Ukraine, ya kunasa makombora yakiwa angani.

Waziri wa ulinzni wa Ujerumani Christine Lambrecht amesema kwamba mitambo hiyo aina ya IRIS-T SLM, itawasili Ukraine katika siku chache zijazo.

"Misururu ya makombora iliyovurumishwa na Russia dhidi ya Ukraine inaonyesha umuhimu wa kutoa msaada wa ulinzi wa anga kwa Ukraine haraka iwezekanavyo,” amesema Lambrecht.

Makombora ya masafa marefu yaliyorushwa na Russia Jumatatu asubuhi, yameua rai ana kuharibu mfumo wa umeme katika sehemu kadhaa za Ukraine. Shambulizi hilo limejiri baada ya rais wa Russia Vladmir Putin kutangaza shambulizi lililotokea kwenye daraja linalounganisha Russia na Crimea, kuwa la kigaidi.

Biden amekemea shambulizi la Russia

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika vita Luhansk, mashariki mwa Ukraine. Jan 28 2022
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika vita Luhansk, mashariki mwa Ukraine. Jan 28 2022

Rais wa Marekani Joe Biden ameshutumu Russia kwa kushambulia Ukraine kwa makombora ya masafa marefu, na kusema kwamba makombora hayo yalilenga raia.

Biden ametangaza kwamba Marekani na washirika wake wataendelea kuiwekea Russia vikwazo kutokana na vita vyake nchini Ukraine.

"Marekani inashutumu kwa nguvu zote mashambulizi ya makombora dhidi ya Ukraine hii leo katika sehemu mbalimbali za Ukraine ikiwemi mjini Kyiv. Mashambulizi hayo yameua rai ana kuharibu mifumo ya nchi bila faida yoyote ya kijeshi,” amesema Biden.

Marekani imetoa msaada wa zaidi yad ola bilioni 16.8 kwa Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza Februari 24.

Marekani na washirika wake vile vile wamewekwa Russia vikwazo kadhaa za uchumi.

"Mashambulizi haya yanaoneza nguvu za kuendelea kuisaidia Ukraine hadi vita vitakapomalizika,” amesema Biden.

Wanajeshi wa Russia wameingia kabisa mashariki mwa Ukraine

Wanajeshi wa Ukraine katika kijiji cha Shandrygolovo, karibu na Lyman, Ukraine. Oct 4 2022
Wanajeshi wa Ukraine katika kijiji cha Shandrygolovo, karibu na Lyman, Ukraine. Oct 4 2022

Taarifa za ujasusi za Uingereza zinasema kwamba wanajeshi wa Russia wamepiga hatua kubwa na kuingia katika mji wa Bakhmut, mashariki mwa Ukraine. Wanajeshi hao wamesonga kilomita 2 kutoka sehemu walikuwa wiki iliyopita.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba Russia inaendelea kupigana kutaka kudhibithi katikati mwa Donbas, hasa sehemu zilizo karibu na mji wa Bakhmut.

Katika ujumbe wa video alioutoa jumamosi, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskit amesema kwamba wanajeshi wa Ukraine wanapambana na wanajeshi wa Russia karibu na mji wa Bakhmut.

Mji wa Bakhmut upo kwenye barabara inayoelekea katika miji ya Sloviansk na Kramatorsk, katika eneo la viwanda la Donabs.

Russia inataka kudhibithi Donbas.

Poland inakagua usalama wa sehemu zake za watu kujificha dhidi ya mabomu

Mgari yakiungua moto kufuatia shambulizi dhidi ya kiwanda cha mafuta katika sehemu inayodhibitiwa na Russia ya Makiivka, mashariki mwa Donetsk, mashariki mwa Ukraine. May 4 2022
Mgari yakiungua moto kufuatia shambulizi dhidi ya kiwanda cha mafuta katika sehemu inayodhibitiwa na Russia ya Makiivka, mashariki mwa Donetsk, mashariki mwa Ukraine. May 4 2022

Nchini Poland, polisi wanakagua ubora wa sehemu za watu kujificha dhidi ya mashambulizi ya mabomu.

Maafisa wa Poland, ambayo ni mwanachama wa NATO, wameambia raia wake kwamba wapo salama kutokana na nchi hiyo kuwa mwanachama wa NATO na kwamba hawawezi kuvamiwa na Russia, lakini inajitayarisha endapo Russia itaishambulia kwa makombora.

"Tuna sehemu 62,000 za kujikinga dhidi ya mashambulizi ya mabomu,” amesema waziri wa mambo ya ndani wa Poland Maciej Wasik.

Serikali ya Poland imeambia raia wake walio Belarus kuondoka nchini humo. Hii ni mara ya pili kwa Poland kutaka raia wake kuondoka Belarus huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kuharibika kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

“Tunawashauri raia wa Poland wanaoishi katika jamhuri ya Belarus kuondoka haraka iwezekanavyo, wakitumia usafiri ulio karibu,” inasema taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa serikali ya Poland.

Putin kukutana na Erdogan

Rais wa Uturuki Erdogan na Putin wa Russia walipokutana Sochi
Rais wa Uturuki Erdogan na Putin wa Russia walipokutana Sochi

Rais wa Russia Vladmir Putin, amepanga kukutana na mwezake wa Uturuki Recep Tayip Erdogan wiki hii, kujailiana kuhusu pendekezo la Uturuki la kufanyika mazungumzo kati ya Russia na mataifa ya magharibi, kuhusu Ukraine.

Msemaji wa Russia Dmitry Peskov, ameambia waandishi wa habari kwamba Russia haijapata ishara yoyote ya kufanyika mazungumzo na mataifa ya magharibi, lakini hajakanusha ripoti kwamba Putin atajadiliana hoja hiyo na Erdogan, watakapokutana.

Putin na Erdogana wanatarajiwa kukutana wiki hii nchini Kazakhstan.

Uturuki ina uhusiano mzuri na Russia Pamoja na Ukraine na imeonekana kuwa mpatanishi anayefaa katika kumaliza vita vya Ukraine.

Uturuki ilisaidia kupatikana makubaliano ya kusafirisha nafaka kutoka Ukraine mwezi July.

XS
SM
MD
LG