Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:54

Afrika katika hatari kubwa ya ukosefu wa chakula baada ya Russia kujiondoa kwenye mkataba


Meli ya kubeba nafaka iliyokodishwa na Sierra Leone, ikiwa katiba black sea, Aug 3, 2022
Meli ya kubeba nafaka iliyokodishwa na Sierra Leone, ikiwa katiba black sea, Aug 3, 2022

Dunia inakabiliwa na hatari ya kutokea uhaba mkubwa wa chakula kufuatia hatua ya Russia kujiondoa kwenye makubaliano ya usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine.

Hatua hiyo inatarajiwa kuziathiri zaidi nchi zinazotegemea uagizaji wa chakula, na huenda ikapelekea dunia kuingia katika hali ya uhaba mkubwa wa chakula na kupanda kwa bei ya nafaka.

Maelfu ya tani za ngano zimezuiliwa bandarini, kwenye meli ambazo tayari zilikuwa zimepakiwa kuelekea Afrika na Mashariki ya Kati.

Russia ilijiondoa kwenye makubaliano ya kusafirisha nafaka siku ya Jumamosi.

Makubaliano hayo yalisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki.

Russia imedai kwamba hatua yake inafuatia shambulizi lililotekelezwa na Ukraine dhidi ya meli zake katika Black Sea.

Bei ya ngano na mahindi ilipanda kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika muda wa miaka 10, mapema mwaka huu, Russia ilipoivamia Ukraine mwezi Februari.

Hakuna meli yenye nafaka imeruhusiwa kuondoka Ukraine tangu Jumapili.

Umoja wa Ulaya, Uturuki na Ukraine wamekubaliana kuendelea kutekeleza mkataba wa usafirishaji wa nafaka.

Meli 16 zinatarajiwa kuodnoka Ukraine leo Jumatatu licha ya kujiondoa kwa Russia.

XS
SM
MD
LG