Wakati shehena za nafaka kutoka bandari za Ukraine hadi maeneo mengine duniani zilianza tena Jumatatu baada ya kusimama kwa muda siku iliyotangulia, wataalam wana wasiwasi kwamba kuvunjika kwa mpango huo kunaweza kusababisha usumbufu wa siku zijazo ambao utaongeza bei zaidi.
Kutokuwa na uhakika mpya kuhusu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kunakuja wakati ambapo mashirika ya misaada duniani kote, ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), yanaonya kuhusu mzozo mkubwa wa njaa duniani.