Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:52

Russia inatumia ‘bomu chafu’ kama kisingizo cha kuendelea kuishambulia Ukraine


Jenerali Sergei Surovikin anayeongoza mashambulizi ya Russia nchini Ukraine. Okt. 8, 2022.
Jenerali Sergei Surovikin anayeongoza mashambulizi ya Russia nchini Ukraine. Okt. 8, 2022.

Mataifa ya Magharibi yameishutumu Russia kwa kutumia kisingizio cha matumimizi ya bomu la nuclear, kuendelea kushambulia Ukraine.

Russia imeendelea kuwaondoa raia kutoka Kherson, mji ulio kusini mwa Ukraine, kwa matarajio ya kutokea mapigano makali.

Utawala wa Moscow umewaambia watu katika mji wa Kherson kuondoka haraka iwezekanavyo na kwamba wanajeshi wake wamewazuia wanajeshi wa Ukraine kuingia sehemu ambazo wanazidhibiti.

Viongozi walioteuliwa na Russia kusimamia Kherson, wametangaza kuundwa kwa kundi la wapiganaji, na kwamba wanaumme wote waliosalia mjini humo watajiunga na wanajeshi katika mapigano.

Ukusanyaji maoni uliofanyika kati ya tarehe 21 na 23 mwezi Oktoba, unaonyesha kwamba raia wa Ukraine wanataka wanajeshi wao waendelee kupigana na wanajeshi wa Russia.

Maoni yalikusanywa wiki mbili baada ya Russia kushambulia miji ya Ukraine kwa makombora.

Bomu chafu

Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, amezungumza na wenzake wa mataifa ya Magharibi Jumatatu na kuwaambia kwamba Moscow inashuku kwamba Kyiv ina[mpango wa kutumia kile ambacho amekiita kuwa “bomu chafu”. Hakutoa ushahidi wowote.

Uingereza, Ufaransa na Marekani zimesema kwamba zitaendelea kuisaidia Ukraine kwa kila hali katika vita hivyo hata kama vitachukua muda mrefu, na kufutilia mbali madai ya Russia kuhusiana na ‘bomu chafu’.

Kamanda wa jeshi la Russia Valery Gerasimov, amefanya mazungumzo na wenzake wa Uingereza na Marekani hii leo, Jumatatu.

Maafisa wa kijeshi wa Marekani wamewaambia waandishi wa habari kwamba Marekani haijaona ishara yoyote kwamba Russia imeamua kutumia silaha za nyuklia, kibaolojia au kemikali.

Iran nayo imekataa kabisa hatua ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza madai kwamba Russia inatumia ndege zisizo na rubani za Iran.

Usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba “kuna mambo mengi yanastahili kufanyika” ili kusafirisha nafaka zaidi kutoka Ukraine.

Zaidi ya meli 150 zinazoshiriki katika usafirishaji wa nafaka katika Black Sea kulingana na mkataba wa usafirishaji wa nafaka hiyo zimekwama.

Mkataba wa kusafirisha nafaka kutoka Ukraine ulipatikana katika mazungumzo yaliyosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa.

Ukraine imesema kwamba meli saba zimeondoka katika bandari zake zikiwa zimebeba nafaka kuelekea Asia na Ulaya, lakini imeilaumu Russia kwa kuzuia utekelezaji wa mkataba wa kusafirisha nafaka hizo.

XS
SM
MD
LG