Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 22:38

Ukraine imefanya mashambulizi mapya Jumapili katika mji wa Kherson


Maisha katika mji wa Kherson ambao ulikuwa unakaliwa na jeshi la Russia Mei 2022. Picha kwa hisani ya VOA Ukrainian
Maisha katika mji wa Kherson ambao ulikuwa unakaliwa na jeshi la Russia Mei 2022. Picha kwa hisani ya VOA Ukrainian

Ukraine ilifanya mashambulizi mapya Jumapili ya kurudisha ardhi karibu na mji wa bandari wa kusini wa Kherson.

Vikosi vya Russia vililenga maeneo huko mashariki mwa Ukraine katika jaribio la kuuteka mji wa Sievierodonetsk mji wa mwisho unaodhibitiwa na Ukraine katika mkoa wa Luhansk.

Kherson unatumika kama uwanja wa kuyatayarisha majeshi ya Russia huko kusini mwa Ukraine mji wa kwanza mkubwa kuangukia kwa wanajeshi wa Moscow waliposonga kaskazini kutoka Crimea zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Lakini Jumapili jeshi la Ukraine lilisema kwenye Twitter subirini Kherson tunakuja. Wakati huo huo Sievierodonetsk ilikuwa lengo kuu la mashambulizi ya Moscow na sasa iko katika mashambulizi makubwa.

Gavana wa eneo la Luhansk ambalo ni pamoja na Donetsk linalounda mkoa wa Donbas alisema Ijumaa kwamba wanajeshi wa Russia wameingia Sievierodonetsk.

Kama Russia ingefaulu kuchukua maeneo haya kuna uwezekano mkubwa ikaonekana kuwa Kremlin imepata mafanikio makubwa ya kisiasa na kuonyeshwa kwa watu wa Russia kama kuhalalisha uvamizi huo wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi.

XS
SM
MD
LG