Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:29

Ukraine inasema imezima mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Russia


Mfano wa ndege zisizotumia rubani (Photo by AFP)
Mfano wa ndege zisizotumia rubani (Photo by AFP)

Jeshi la anga la Ukraine limesema ulinzi wake wa anga uliziangusha ndege zote nane zilizorushwa na Russia

Jeshi la Ukraine limesema Jumatatu kuwa limezima mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Russia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo usiku wa kuamkia leo, huku maafisa wa Russia wakivishutumu vikosi vya Ukraine kwa kufanya shambulizi la kiovu katika mji wa mashariki mwa Ukraine unaodhibitiwa na Russia.

Jeshi la anga la Ukraine limesema ulinzi wake wa anga uliziangusha ndege zote nane zisizokuwa na rubani zilizorushwa na Russia, ikiwemo katika anga kwenye mikoa ya Mykolaiv, Kherson na Dnipropetrovsk.

Huko Moscow, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Ukraine ilitumia kiholela silaha na kushambulia miundombinu ya raia wakati wa mashambulizi ya makombora siku ya Jumapili katika mji wa Donestk na kuua watu wasiopungua 27.

Peskov pia alisema Jumatatu kwamba Russia inachukua hatua muhimu baada ya shambulio linalodhaniwa kufanywa na Ukraine kwenye kituo cha kusafirisha mafuta kwenye Bahari ya Baltic. Jeshi la Ukraine halikutoa tamko lolote hadharani kuhusu shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG