Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:48

Umoja wa Ulaya wasema utaongeza uzalishaji wa silaha kuitikia wito wa Ukraine


Bendera za Umoja wa Ulaya katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels. REUTERS
Bendera za Umoja wa Ulaya katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels. REUTERS

Umoja wa Ulaya ulisema Ijumaa kuwa utaongeza uzalishaji wake wa silaha  kuitikia wito wa Ukraine wa kuungwa mkono huku vita vyake dhidi ya Russia vikikaribia katika kipindi cha miaka miwili.

Ifikapo mwisho wa mwaka, Kamishna wa Soko la Ndani la Umoja wa Ulaya Thierry Breton alisema, EU itaweza kuzalisha takriban risasi milioni 1.3.

Tuko katika wakati muhimu kwa usalama wetu wa pamoja barani Ulaya, na katika vita vya kichokozi vinavyoendeshwa na Russia nchini Ukraine, Ulaya lazima na itaendelea kuiunga mkono Ukraine kwa kila njia Breton aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake huko Estonia.

Forum

XS
SM
MD
LG