Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:50

Maafisa wa White House wajadili namna ya kuisaidia Ukraine kwa teknolojia mpya


Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa White House.
Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa White House.

Uwezo wa kiteknolojia utakaoiruhusu Ukraine kugundua na kukabiliana na mifumo ya anga isiyo na rubani ya Russia.

Maafisa wa White House walikutana Jumatatu na viongozi kutoka sekta ya teknolojia na ulinzi kujadili jinsi ya kuipa Ukraine vifaa vya hali ya juu vya Marekani kama vile mifumo ya angani isiyo na rubani au vifaa vya kutungua makombora na kuisaidia katika juhudi zake za kujilinda dhidi ya Russia, kulingana na wasaidizi wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani.

Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa White House, aliitisha mkutano wa saa tano kati ya wataalam wa sekta hiyo na maafisa wa serikali juu ya uwezo mpya wa kiteknolojia ambao utairuhusu Ukraine kugundua na kukabiliana na mifumo ya anga isiyo na rubani ya Russia inayoharibu maeneo makubwa nchini Ukraine, kama mfuko wa misaada ya ziada wa Rais Joe Biden wa zaidi ya dola bilioni 100, ambao unajumuisha msaada kwa Ukraine, unakwamishwa katika Bunge.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya siku ya Jumatatu kutoa msaada zaidi wa kijeshi na kifedha kwa Ukraine. Alizikosoa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kwa kutotoa silaha za kutosha kwa Kyiv na kuwataka kufanya zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG