Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:18

Putin aapa kusogeza vikosi vya Ukraine mbali na mpaka wake


Rais wa Russia Vladimir Putin.
Rais wa Russia Vladimir Putin.

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano ameapa kusukuma nyuma vikosi vya Ukraine, ili kupunguza tishio la kushambuliwa kwa eneo la Russia, wakati alipokuwa akikutana na wanaharakati wanaoendesha kampeni zake, kabla ya uchaguzi wa rais utakaofanyika Machi, na ambao ana uhakika wa kushinda.

Alipoulizwa kuhusu mpango wake wa mashambulizi ya kijeshi ndani ya Ukraine, Putin alisema kwamba, wanajeshi wa Ukraine wanahitaji kusukumwa nyuma, kiasi kwamba silaha za masafa marefu kutoka magharibi zinazotumiwa na Ukraine, hazitaweza kufikia miji yenye amani ndani ya Russia. Aliongeza kusema kwamba kwa muda wote huu, jeshi lake limekuwa likitekeleza hilo.

Ukraine katika siku za karibuni imefanya mashambulizi ndani ya Russia, likiwemo lile la Desemba 30 kwenye mji wa mpakani wa Belgorod, lililouwa watu 25 na kujeruhi wengine zaidi ya 100. Putin pia ameongeza kusema kwamba wachunguzi wamedhibitisha kwamba Ukraine ilitumia mfumo wa ulinzi wa anga aina ya Patriot kutoka Marekani, kuangusha ndege ya kijeshi karibu na Belgorod, hapo Januari 24.

Forum

XS
SM
MD
LG