Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:39

Biashara ya kimataifa yavurugwa na mashambulizi Bahari ya Sham na vita vya Ukraine


Wapiganaji wa Kihouthi wakionyesha silaha zao kupinga mashambulizi yaliyofanywa na majeshi ya Marekani an Uingereza katika mji uliokuwa chini ya mamlaka ya Wahouthi huko Sanaa.
Wapiganaji wa Kihouthi wakionyesha silaha zao kupinga mashambulizi yaliyofanywa na majeshi ya Marekani an Uingereza katika mji uliokuwa chini ya mamlaka ya Wahouthi huko Sanaa.

Shirika la  biashara ya Umoja wa Mataifa limesema Alhamisi kuwa biashara ya kimataifa inavurugwa na mashambulizi katika Bahari ya Sham, vita vya Ukraine, na kiwango cha chini cha maji katika Mfereji wa Panama.

Jan Hoffman, mtaalam wa biashara katika shirika la UN la UNCTAD, ameonya kuwa gharama za usafirishaji zitaongezeka, na gharama za nishati na chakula tayari zimeathirika, ikiongeza hatari za mfumuko wa bei.

Tangu mashambulizi yanayofanywa na waasi wa Kihouthi wa Yemen dhidi ya meli katika Bahari ya Sham yaliyoanza Novemba, alisema, wahusika wakubwa katika sekta ya usafirishaji wa baharini wamesitisha kwa muda kutumia mfereji wa Suez, sehemu muhimu ya kuingia katika Bahari ya Mediterranean kuelekea Bahari ya Sham na njia muhimu kwa usafirishaji nishati na mizigo kati ya Asia na Ulaya.

Mfereji wa Suez unapitisha biashara za kimataifa za asilimia 12 na 15 mwaka 2023, lakini UNCTAD inakadiria kuwa kiwango cha biashara kinachopita katika mlango huo wa bahari imepungua kwa asilimia 42 katika miezi miwili iliyopita, Hoffmann alisema.

Tangu mwezi Novemba, Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wamefanya mashambulizi yasiyopungua 34 dhidi ya meli katika njia inayoelekea Mfereji wa Suez.

Wahouthi hao, kikundi cha waasi wa Kishia ambacho kimekuwa katika vita na ushirika wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia ambao wanaiunga mkono serikali ya Yemen iliyoko uhamishoni tangu mwaka 2015, wanawaunga mkono Wapalestina na wameapa kuendelea kushambulia meli mpaka pale vita ya Israel – Hamas vitapomalizika.

Marekani na Uingereza zimejibu kwa mashambulizi dhidi ya malengo ya Wahouthi, lakini waasi hao wameendeleza mashambulizi yao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG