Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:15

Yemen: Kombora laigonga meli ya mafuta ya Norway


FILE - Mlango wa Bahari ya Bab al-Mandab, linalodhibitiwa na Wahouthi ambapo meli ya Norway ilishambuliwa kwa kombora.
FILE - Mlango wa Bahari ya Bab al-Mandab, linalodhibitiwa na Wahouthi ambapo meli ya Norway ilishambuliwa kwa kombora.

Kombora lililorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen liliigonga meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Norway katika mlango wa bahari wa  Bab al-Mandab siku ya Jumanne.

Kupitia taarifa kutoka kamandi kuu ya Marekani shambulio hilo lilisababisha moto kwenye meli ya mafuta ya STRINDA, lakini hakuna ripoti za majeruhi.

Shambulio hilo ni la hivi karibuni lililofanywa na wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran ndani au karibu na Bahari ya sham, pamoja na kurusha ndege zisizo na rubani na makombora kuilenga Israel.

Jeshi la Wanamaji la Marekani Jumapili lilitoa video kuonyesha meli katika Bahari sham ikifyatua makombora ili kuzuia mashambulizi kutoka kwa waasi wa kihouthi wa Yemen.

Video hiyo inaishia kwa kuonyesha maandishi USS Carney (DDG 64) 22-0.

Waasi wa kihouthi walisema Jumamosi watazilenga meli zozote zinazoelekea Israel kupitia njia muhimu za meli zinazopita Yemen.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG