Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:59

Rais wa Iran: Vitendo vya Israel 'vinaweza kumlazimisha kila mtu' kuingilia vita hii


FILE - Rais wa Iran Ebrahim Raisi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kupinga vitendo vya Israel katika Viwanja vya Islamic Revolution Square, Tehran, Iran, OKtoba. 18, 2023.
FILE - Rais wa Iran Ebrahim Raisi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kupinga vitendo vya Israel katika Viwanja vya Islamic Revolution Square, Tehran, Iran, OKtoba. 18, 2023.

Israel imekuwa ikilishambulia eneo la Wapalestina tangu Hamas iliupofanya uvamizi wa kuvuka mpaka Oktoba 7 na kuua zaidi ya watu 1,400, wengi wao ni raia, maafisa wa Israeli walisema.

Tangu wakati huo, zaidi ya watu 8,000 wameuawa huko Gaza, nusu kati yao ni watoto, kulingana na wizara ya afya katika eneo linaloendeshwa na Hamas, ukanda ambao ni maskini na makazi ya watu milioni 2.4.

“Uhalifu huo wa utawala wa kizayuni umevuka mstari mwekundu, na hili linaweza kumsukuma kila mtu kuchukua hatua,” Raisi alisema katika mtandao wa X, uliokuwa zamani ukijulikana kama Twitter.

“Washington inatuambia tusifanye chochote, lakini wanaendelea kuwaunga mkono Israel,” alisema.

“Marekani imetuma idadi kadhaa za ujumbe kwa mhimili wa kujihami lakini imepokea jawabu la wazi katika uwanja wa vita,” aliandika, akitumia maneno ambayo aghlabu yanatumiwa na maafisa wa Iran kuielezea Jamhuri ya Kiislam na washirika wake kama vile kikundi cha Hezbollah cha Lebanon, Wahouthi wa Yemen na wapiganaji wengine wa Kishia huko Iraq na Syria.

Ingawaje haikuwa bayana kile alichokuwa anakielezea, kumekuwa na mfululizo wa mashambulizi dhidi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq na Syria na kuongezeka kwa mapambano ya bunduki kati ya majeshi ya Hezbollah na Israeli katika mpaka wa Lebanon tangu vita vya Gaza kuanza.

Iran, ambayo inaiunga mkono Hamas kifedha na kijeshi, ilipongeza shambulizi la Oktoba 7 kuwa la mafanikio.

Lakini imesisitiza kuwa haikuhusika kushiriki katika shambulizi hilo wakati ambapo watu 230 walitekwa nyara, kulingana na mamlaka za Israeli.

“Iran inakadiria kuwa ni jukumu lake kuunga mkono makundi yenye kujihami, lakini … makundi yenye kujihami yanajitegemea katika maoni, maamuzi na vitendo vyao,” rais wa Iran alisema katika mahojiano na televisheni ya Al Jazeera Jumamosi, kulingana na nukuu zilizotolewa na shirika la habari la serikali IRNA.

“Marekani inajua fika kuhusu uwezo wetu wa hivi sasa na wanajua ni vigumu kwao kutudhibiti,” alisema.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG