Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:43

Wakati shambulizi la Hamas dhidi ya Israel likileta wasiwasi Mashariki ya Kati mustakbali wa programu ya nyuklia ya Iran mashakani


Kinu cha Nyuklia cha Iran. Rais wa zamani wa Iran Ahmadi Najed akikagua mradi huo.
Kinu cha Nyuklia cha Iran. Rais wa zamani wa Iran Ahmadi Najed akikagua mradi huo.

Huku hali ya wasiwasi ikitanda Mashariki ya Kati kufuatia shambulizi la Hamas dhidi ya Israel  na mashambulizi ya Israel katika maeneo ya Hamas huko Gaza, Mustakbal wa program ya Nyuklia ya Iran bado haujatatuliwa.

Kama anavyoripoti Henry Ridgwell, Mataifa ya Magharibi yanaiona Tehran kama muungaji mkono mkuu wa Hamas na mashambulizi ya kundi hilo dhidi ya Israel yamerudisha nyuma juhudi za kuzima mivutano na Iran.

Viongozi wa Magharibi wanaiona Iran kama muungaji mkono mkubwa wa kundi la wanamgambo la Hamas lakini hawajaishutumu Tehran kuhusika moja kwa moja na mashambulizi ya kundi hilo la Oktoba 7 dhidi ya Israel.

Kabla ya shambulizi, uhusiano baina ya Mataifa ya Magharibi na Iran ulionekana kuimarika japo kwa tahadhari. Mwezi Septemba, Marekani ilifikia makubaliano ya kubadilishana wafungwa na Tehran na vile vile kuachilia dola billioni 6 za mali ya Iran zilizokuwa zimezuiliwa. Lakini Fedha hizo zikazuiliwa tena.

Kiongozi wa Hezbollah wa Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah akutana na Katibu Mkuu wa kikundi cha Jihad Ziyad al-Nakhalah naibu wa kiongozi wa kikundi cha Hamas, Sheikh Saleh al-Arouri wakikutana katika eneo lisilo julikana.
Kiongozi wa Hezbollah wa Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah akutana na Katibu Mkuu wa kikundi cha Jihad Ziyad al-Nakhalah naibu wa kiongozi wa kikundi cha Hamas, Sheikh Saleh al-Arouri wakikutana katika eneo lisilo julikana.

Ali Vaez, Mchambuzi wa Kundi la International Crisis Group anasema: “ kulikuwa na nafasi kwa mashauriano ya moja kwa moja kumalisa mzozo Mwezi Oktoba kati ya Iran na Marekani nchini Oman. Lakini nadhani hilo kwa sasa halitafanyika tena , pengine hakuna nia ya kisiasa iliyobaki kufanikisha ushirikiano wa moja kwa moja kati ya nchi hizi Mbili.”

Mazungumzo ya Vienna ya kufufua makubaliano ya Nyuklia ya Iran ya 2015 , Mpango wa pamoja wa JCPOA yalikwama mwaka jana japo hakuna upande wowote ambao unakiri kuwa umekamilisha rasmi .

Marekani ilijiondoa katika mkubaliano ya JCPOA mwaka 2018 - na Iran iliacha kutekeleza ahadi zake baada ya hapo.

Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Nyuklia, Shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki, lilisema kwenye ripoti yake ya Agosti kwamba Iran inaendelea kusindika Uranium hadi asilimia 60 ya kiwango cha usafi lakini ina upungufu wa asilimia 90 ya mafuta ya kiwango cha silaha. Iran Imeondoa vifaa vya ukaguzi vya IAEA na kuwazuia baadhi ya wakaguzi kuzuru nchi hiyo.

Vaez ameongeza kuwa: "Huku uhusiano kati Iran na Marekani ukididimia , Iran iliacha kukusanya uranium iliyorutubishwa kwa 60%. Na hiyo inaweza sasa kubadilika kutokana na kuongezeka kwa mivutano kati ya pande hizo mbili. Ingeichukua Iran chini ya wiki moja kurutubisha uranium ya kutosha kwa ajili ya silaha moja ya nyuklia. Na ndio maana hili ni bomu la kutisha na kunahitajika suluhu kwa njia moja au nyingine ili kuzuia athari za nyuklia za Iran.”

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi alisema "hakuna uhusiano" kati ya vita vya Israel na Hamas na mpango wa nyuklia wa Iran.

Rafael Grossi
Rafael Grossi

Peter Jenkins, Balozi wa zamani wa Uingereza katika IAEA anasema: "Bado hakuna ushahidi kwamba Iran inatafakari kuondoka katika utekelezaji wa ahadi yake muhimu ya Mkataba wa Kuzuia kuenea kwa Nyuklia, ambayo ni kujiepusha na utengenezaji wa silaha za nyuklia."

Balozi huyo anaongeza kuwa: “Nafikiria wanaweza kubuni njia za kuongeza wasiwasi katika mataifa ya magharibi kutokana na mpango wao Nyuklia lakini kwa ufupi tunaweza sema ni kuvuka mipaka na kuacha kuzingatia mkataba wa kuzuia unezaji wa Nyuklia”

Wakati huo huo , Israel imesema haitairuhusu Iran Kutegeneza silaha za Nyuklia

Israel yenyewe inaaminika kuwa na silaha za atomiki - ingawa hairuhusu ukaguzi wa IAEA wa maeneo yake ya nyuklia.

Ripoti ya Henry Ridgwell: Imetayarishwa na mwandishi wetu Hubbah Abdi, Washington, DC.

Forum

XS
SM
MD
LG