Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:32

Msafara wa pili wa malori ya misaada waingia Gaza Jumapili


Wafanyakazi wa Misri wakitazama lori likirejea kutoka Gaza baada ya kupeleka msaada.
Wafanyakazi wa Misri wakitazama lori likirejea kutoka Gaza baada ya kupeleka msaada.

Msafara mpya wa malori 17 ya misaada umeingia huko Gaza Jumapili wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake dhidi ya eneo hilo ambalo linapitia hali ngumu ya kibinadamu.

Hali hiyo ni kufuatia vita vilivyosababishwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel hapo Oktoba 7. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Iran imesema kwamba vita hivyo huenda vikasambaa kote kwenye eneo la Mashariki ya Kati, wakati waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu akionya kundi la Hezbollah la Lebanon kwamba litajuta iwapo litaingilia vita hivyo.

Ripoti zinasema kwamba Israel imeuwa zaidi ya wapalestina 4,600 tangu mapigano hayo yalipozuka, wengi wao wakiwa raia, kulingana na wizara ya afya ya Gaza. Umoja wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya asilimia 40 ya nyumba huko Gaza zimeharibiwa na, wakati Israel ikiwa imesitisha huduma muhimu za kibinadamu kama maji, mafuta na umeme.

Msafara wa leo kuingia Gaza kupitia mpaka wa Misri wa Rafah ni wa pili ndani ya siku mbili, wakati mwingine wa malori 20 ukiwa umeingia Jumamosi. UN unakisia kwamba malori takriban 100 yanahitajika kila siku ili kukidhi mahitaji ya wakazi milioni 2.4 wanaoishi Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG