Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:28

Israel yafanya mashambulizi ya Gaza na Syria usiku kucha


Vifaru vya kijeshi vya Israel vikishika doria karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza
Vifaru vya kijeshi vya Israel vikishika doria karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza

Vikosi vya Isreal usiku kucha vimefanya mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza, Syria na kwenye mpaka wa Lebanon, wakati kukiwa na wasi wasi kwamba mzozo kati ya Israel na Hamas huenda ukasambaa kwenye eneo lote la Mashariki ya Kati.

Hamas imesema kwamba takriban watu 55 wameuwawa usiku kucha kutokana na mashambulizi hayo ya Ukanda wa Gaza, ambako Israel imekuwa ikifanya mashambulizi mfululizo tangu kuuwawa kwa takriban watu wake 1,400 mapema mwezi huu na wanamgambo wa Hamas.

Nchini Syria, shirika la habari la serikali la SANA limesema kwamba makombora ya Israel yamegonga viwanja vya ndege kwenye mji mkuu wa Damascus, na kwenye mji wa kaskazini wa Aleppo. Taarifa zimeongeza kusema kwamba mfanyakazi mmoja kwenye uwanja wa ndege ameuwawa huku mwenzake akijeruhiwa.

Safari za ndege nchini humo sasa zimehamishiwa kwenye uwanja wa ndege wa Lattakia. Israel ndani ya mwaka mmoja uliopita imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya viwanja vya ndege vya Damascus na Aleppo, gazeti la The Times of Israel likisema kwamba Israel inaaminika kuzuia upelekaji wa silaha kutoka Iran hadi kwenye washirika wake Mashariki ya Kati, mshirika mkuu akiwa kundi la Hezbollah lenye makao yake Lebanon.

Forum

XS
SM
MD
LG