Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:34

Guterres aomba sitisho la mapigano kati ya Israeli-Hamas kwa misingi ya kibinadamu


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kushoto) na rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kushoto) na rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Jumamosi ameomba kupitishwa “sitisho la mapigano la kibinadamu” katika vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ambavyo vimesababisha vifo vingi na kuharibu sehemu kubwa ya Gaza, akiktaka “hatua kuchukuliwa kumaliza janga hili baya sana.”

Akizungumza katika mkutano wa Cairo, wakati mzozo ukiingia wiki ya tatu, Guterres amesema watu wanaishi katika ‘hali ya janga la kibinadamu’ kenye eneo la Wapalestina lenye takriban watu milioni 2.4, huku maelfu wakiwa wamepoteza maisha na zaidi ya milioni moja hawana makazi.

“Tunakutana katikati ya kanda ambayo imekumbwa na uchungu wa muda mrefu na hatua moja kutoka kwenye majanga,” aliuambia mkutano huo ambao uliwajumuisha viongozi wa Misri, Iraq, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja Umoja wa Ulaya na rais wa Palestina Mahmud Abbas.

Umwagaji damu ulianza Oktoba 7 wakati wanamgambo wa Hamas walivuka mpaka wa Gaza na kuingia Israel, na kuanzisha mashambulizi ambayo yaliua zaidi ya watu 1,400, wengi wao raia, katika shambulizi baya sana kwenye ardhi ya Israel tangu taifa hilo kuanzishwa mwaka 1948.

Mkutano wa Kilele wa Cairo kwa ajili ya Amani unafanyika katika hoteli St Regis Almasra mjini Cairo
Mkutano wa Kilele wa Cairo kwa ajili ya Amani unafanyika katika hoteli St Regis Almasra mjini Cairo

Guterres alisema “umalalamiko ya watu wa Palestina ni halali na wa muda mrefu” baada ya “miaka 56 ya ukaliaji wa kimabavu bila ya mwisho kuonekana” lakini alisisitiza kwamba “hakuna kinacho halalisha shambulizi baya sana lililofanywa na Hamas ambalo limewatia khofu raia wa Israel.”

Baadaye alisisitiza kwamba “mashambulizi hayo ya kuchukiza hayawezi kamwe kuhalilisha adhabu ya jumla kwa watu wa Palestina.”

Mfalme Abdulla wa II wa Jordan aliomba “kumalizwa haraka kwa vita huko Gaza” na kulaani kile alichokitaja “ukimya wa ulimwengu” kwa vifo vya wapalestina na maafa.

“Ujumbe wa dunia ya Kiarabu unasikika kwa sauti na wa wazi: Maisha ya Wapalestina hayajaliwi sana kwama ya Waisraeli. Maisha yetu yanajaliwa kwa uchache sana kuliko maisha ya wengine,” alisema.

“Matumizi ya sheria ya kimataifa ni hiari. Na haki za binadamu zina mipaka – zinaishia kwenye mipaka, zinaishia kwenye ushindani, na zinaishia kwenye dini.”

Mkutano umefanyika siku ile ile msafara wa malori ya misaada ukielekea kusini mwa Gaza, ambako Guterres amesema kuna haja ya kuongeza misaada kwa haraka sana, huku “msaada mwingi zaidi” unahitaji kupelekwa.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba kiasi cha magari 100 kwa siku yanahitajika ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka huko Gaza.

Wapalestina wanahitaji "kupelekwa kwa misaada isio sita huko Gaza kwa kiwango ambacho kinahitajika”, mkuu wa Umoja wa Mataifa aliuambia “Mkutano wa Amani” mjini Cairo.

Forum

XS
SM
MD
LG