Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:17

Jumuiya ya Kimataifa yalaani shambulio dhidi ya hospitali mjini Gaza


Wapalestina walojeruhiwa kutokana na shambulio kubwa kwenye hospitali ya Al-Ahli Arab, Gaza
Wapalestina walojeruhiwa kutokana na shambulio kubwa kwenye hospitali ya Al-Ahli Arab, Gaza

Jumuia ya Kimataifa imeshtushwa na shambulio dhidi ya hospitali ya Al Ahil Arab, mjini Gaza City na mara moja kulaani vikali kitendo hicho.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterees akizungumza kwenye mkutano wa kilele wa uwekezaji wa Belt and Road mjini Bejing, siku ya Jumatano alisema mashambulio ya Hamas dhidi ya Israel haihalalishi “adhabu ya pamoja” dhidi ya Wapalestina na kutoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa tatu wa Belt and Road Forum kwa ajili ya Ushirikiano wa Kimataifa mjini Bejing.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa tatu wa Belt and Road Forum kwa ajili ya Ushirikiano wa Kimataifa mjini Bejing.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa Hamas kuwaachilia huru mateka mara moja, bila ya masharti yeyote, akizungumzia karibu watu 199 wanaoshikiliwa na Hamas. Na kutaka msaada wa dharura kupelekwa katika Ukanda wa Gaza mara moja.

Mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, Faki Mahamat ameituhumu Israel kwa “uhalifu wa vita” kufuatia shambulio hilo lililolsababisha vifo vingi.

Katika ujumbe wake anasema hakuna maneno yanayoweza kueleza kitendo hicho isipokua kulaani vikali kitendo cha kushambulia hospitali na raia mjini Gaza.

Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Charles Michael amesema ni jambo la kusikitisha sana kwa miundombinu ya raia kulengwa huko Gaza na ina kiuka kabisa sheria za kimataifa.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa dharura wa Umoja wa Ulaya.

Anasema shambulio dhidi ya miundombinu ya raia linakiuka kabisa sheria za kimataifa.

Mataifa mengine ya kiarabu ikiwa ni pamoja na Jordan, Qatar, Tunisia, Lebanon na Uturuki yamelaani kitendo hicho wakieleza ni cha kikatili.

Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadam ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk ameeleza shambulio la hospitali kuwa ni jambo lisilokubalika hata kidogo, akisisitiza kwamba walohusika na kitendo hicho ni lazima wawajibishwe.

Shirika la Afya Duniani WHO, limelaani shambulio hilo na kutaka mara moja raia kulindwa pamoja na kutoshambulia hospitali kwenye Ukanda wa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG