Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:55

Katibu mkuu wa UN ashinikiza misaada ipelekwe Gaza


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry wafanya mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wao mjini Cairo, Oktoba 19, 2023.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry wafanya mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wao mjini Cairo, Oktoba 19, 2023.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres Ijumaa amesafiri kuelekea mji wa Misri wa Sinai katika jitihada za kuruhusu misaada kuingia ndani ya eneo la Palestina lililozingirwa la Gaza, lakini haijafahamika ni lini usambazaji wa misaada iliyopo nchini Misri utaanza.

Mjini Geneva, ofisi ya Umoja wa mataifa ya misaada ya kibinadamu ilisema iko katika mazungumzo na pande zote katika mzozo kati ya Israel na Hamas ili kuhakikisha operesheni ya kupeleka misaada inaanzishwa hivi karibuni huko Gaza.

Marekani ilisema maelezo ya makubaliano ya kupeleka misaada kupitia mpaka wa Rafah kati ya Misri na Gaza bado yanaendelea kuboreshwa.

Awali, Washington ilisema makubaliano ya kupitisha kwenye mpaka huo lori za kwanza 20 yalifikiwa, lakini maafisa wa Umoja wa mataifa wanasema kwamba usambazaji wowote wa misaada unastahili kufanywa kwa awamu na kwa njia endelevu.

Kabla ya mzozo wa hivi sasa kati ya Israel na Hamas kuzuka, takriban malori 450 ya misaada yalikuwa yanaingia kila siku Gaza.

Wengi kati ya wakazi milioni 2.3 wa Gaza wanategemea misaada ya kibinadamu. Eneo hilo la pwani limekuwa chini ya vikwazo vilivyowekwa na Israel na Misri tangu Hamas ilipolidhibiti mwaka wa 2007.

Forum

XS
SM
MD
LG