Akizungumza kwenye kongamano la uchumi nchini China Jumatano, Guterres amelaani shambulizi la Hamas ambalo liliua watu 1,400 nchini Israel akisema ni ‘kitendo cha kigaidi’, ambacho hakiwezi kuhalalishwa.
Guterres ameitaka Hamas haraka sana kuwaachilia bila masharti takriban mateka 199 waliochukuliwa wakati wa tukio hilo lililotajwa kuwa baya sana katika historia ya Israel. Guterres pia ameiomba Israel kuruhusu haraka sana fursa ya kupitisha misaada ya kibinadamu kwenda Gaza ambako wengi wanaoumia ni wanawake na watoto.
Amesema kwamba anafahamu malalamiko ya watu wa Palestina baada ya ardhi yao kukaliwa kwa miaka 56. Awali Guterres alisema alishtushwa na mlipuko mbaya uliotokea Jumanne kwenye hospitali ya Gaza na kuua mamia ya watu.
Forum