Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:59

Wasiwasi wa kuzuka vita vipana Mashariki ya Kati wazidi kuongezeka


Meli ya mashambulizi ya Marekani USS Bataan ikiwa safarini katika Bahari ya Red Sea on Aug. 8, 2023.
Meli ya mashambulizi ya Marekani USS Bataan ikiwa safarini katika Bahari ya Red Sea on Aug. 8, 2023.

Wasiwasi wa kuzuka kwa vita vipana  Mashariki ya Kati unazidi kuongezeka, huku Marekani ikituma vifaa zaidi vya kijeshi  na kuonya kuhusu vitisho kwa Wamarekani na vituo vya Marekani katika eneo hilo.  

Jeshi la Israel limeongeza mashambulizi ya anga huko Gaza na kuharibu maeneo kadhaa huku kukiwa na matarajio ya kufanyika kwa mashambulizi ya ardhini.

Kuna hofu ya vita vipana zaidi kuzuka, Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa Marekani, John Kirby, amesema mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani yameongezeka katika eneo hilo.

FILE PHOTO: John Kirby
FILE PHOTO: John Kirby

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa, ,Marekani anaeleza: " Tunajua Iran inawaunga mkono Hamas na Hezbollah. Na tunajua kuwa Iran inafuatilia kwa kina matukio haya ,na katika baadhi ya matukio , inafadhili mashambulizi haya na kuwachochea wengine ambao wanataka kujinufaisha na mgogoro huu kama Iran.

Tunajua lengo la Iran ni kuendelea kudai kuwa hawahusiki hapa, lakini hatuta kubali waendele kufanya hivyo, Na pia hatutakubali vitisho vyovyote kwa maslahi yetu katika eneo hilo bila ya kushutumiwa.

Jumapili waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alizungumza na kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week,” na kusema kuwa marekani itaongeza uwepo wake wa kijeshi huko mashariki ya Kati.

Lloyd Austin, Waziri wa Ulinzi wa Marekani ameeleza: “Kama mnavyojua kumekuwa na mashambulizi ya roketi na UAV kwenye kambi za kijeshi nchini Iraq na Syria. Tuna wasiwasi wa kuongezeka kwa vita . Kwa hakika kile tunachokiona ni kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wetu na watu wetu katika eneo hilo. kwa sababu hiyo tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa wanajeshi wetu wako tayari na wanalindwa."

Lloyd Austin
Lloyd Austin

Tangu mashambulizi haya kuanza Okotoba 7 Kusini mwa Israel yaliyofanywa na kundi la Hamas, na kuua zaidi 1400, Israel ilifanya mashambulizi huko Gaza na kusababisha vifo vya wapalestina 5000.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya Kibinadamu yametoa wito wa kusitishwa kwa vita kwa ajili ya kibinadamu . Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mathew Miller alikuwa na haya ya kusema Jumatatu:Sitisho lolote la mapigano litaipa Hamas nafasi ya kumpuzika katika vita, kujipanga na kuwa tayari kuendeleza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Israel."

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel alisema Jumatatu kuwa aliamini viongozi wa kundi hilo wangekubali kusitisha vita kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Misaada ya kibinadamu iliendelea kuingia Gaza huku malori ya misaada 20 yakiingia. Hata hivyo ukosefu wa mafuta kwa ajili ya usafirishaji huenda ukasitisha operesheni hiyo huku Wapalestina zaidi ya millioni mbili waliozingirwa wakisubiri misaada.

Ni Ripoti ya Mwandishi wa VOA wa masuala ya diplomasia Cindy Saine, Imetayarishwa na Hubbah Abdi, Washington, DC.

Forum

XS
SM
MD
LG