Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:33

Wanajeshi wa Israeli wavamia nyumba ya kiongozi mwandamizi wa Hamas, wawaweka kizuizini wanafamilia


Saleh al-Aruri
Saleh al-Aruri

Wanajeshi wa Israeli Jumamosi walivamia nyumbani kwa kiongozi mwandamizi wa Hamas katika Ukingo wa Magharibi na kuwaweka kizuizini watu wa familia yake, walioshuhudia walisema.

Saleh al-Aruri ni naibu wa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh, na mmoja wa waanzilishi wa tawi la kijeshi la kundi hilo la Kiislamu.

Mkazi wa Lebanon, ndiye mlengwa mkuu wa Israel kufuatia mashambulizi ya Oktoba 7 wakati wapiganaji wa Hamas kutoka Gaza walipovamia kusini mwa Israeli na kuua takriban watu 1,400, wengi wao wakiwa ni raia na kuwateka zaidi ya 200, kwa mujibu wa maafisa wa Israeli.

Tangu wakati huo, zaidi ya Wapalestina 4,300, hasa raia, wameuawa katika mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel, kulingana na wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.

Wanajeshi waliingia nyumbani kwa Aruri katika kijiji cha Arura, takriban kilomita 20 kaskazini mwa Ramallah, alfajiri ya Jumamosi, na kuwakamata zaidi ya watu 20, akiwemo mmoja wa kaka zake na wapwa zake tisa, meya Ali al-Khasib na mashahidi waliliambiambia AFP.

Darzeni wengine wanashikiliwa kwa mahojiano.

Forum

XS
SM
MD
LG