Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 17:22

Jakarta na Kuala Lumpa wamekusanyika kupinga vita vinavyoendelea Gaza


Washiriki katika maandamano hayo walichoma na kukanyaga bendera za Israel na picha ya Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Huko Kuala Lumpa waandamanaji walizuiwa na polisi kuandamana kuelekea jengo la ubalozi wa Marekani

Mamia ya watu huko Jakarta na Kuala Lumpa walikusanyika kwenye ubalozi wa Marekani hii leo baada ya sala ya Ijumaa na kuchoma bendera za Israel ili kuonyesha mshikamano kwa wa-palestina huko Gaza.

Washiriki katika maandamano hayo walichoma na kukanyaga bendera za Israel na picha ya Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Huko Kuala Lumpa waandamanaji walizuiwa na polisi kuandamana kuelekea jengo la ubalozi wa Marekani.

Waandamanaji katika nchi zote mbili walisema mlipuko katika hospitali ya Gaza ambao wa-Palestina walilaumu kuwa ni shambulizi la anga lililofanywa na Israel lakini Israel ilisema lilisababishwa na roketi iliyorushwa lakini iliyofeli na kusema ni ya wanamgambo wa Palestina.

Biden aliunga mkono madai ya Israel.

Wizara ya afya ya Gaza imesema wa-Palestina 3,478 wameuawa na 12,065 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye eneo lililozingirwa tangu Oktoba 7 kufuatia shambulio kwa Israel lililofanywa na wanamgambo wa Hamas wenye makao yake huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG