Rais Joe Biden ametoa ombi la moja kwa moja kwa wamarekani kuendelea kuifadhili Ukraine na Israel katika juhudi zao za vita, aliyasema hayo akiwa ofisini kwake akitoa hotuba Alhamisi usiku, siku moja baada ya kurejea kutoka Tel Aviv kuonyesha uungaji mkono kwa mshirika mkuu wa Washington.
Wapalestina wasiokuwa na makazi wamejikusanya kwenye mahema kusini mwa Gaza wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake ya anga ambayo yamefanya msikiti katikati ya Gaza katika mji wa Deir al Balah kuwa kifusi. Hii imetokea baada ya matamshi ya Rais Joe Biden Alhamisi usiku, akiwa amerejea tu kutoka Tel Aviv, akiomba ufadhili zaidi kwa Israel, mshirika mkuu wa Marekani, pia uungaji mkono kwa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia. “Hamas na Putin wanaleta vitisho tofauti, lakini mtizamo wao ni mmoja. Wote wanataka kuiangamiza kabisa demokrasia kwa jirani yao.”
Israel imeishambulia kwa mabomu Gaza, na kuua watu 3,000 na kuwakosesha makazi zaidi ya milioni moja, wengi wao waarabu wakipalestina,
Ikiwa ni majibu kwa uvamizi wa Oktoba 7 uliofanywa na kundi la Hamas, ambao uliuua watu 1,400 ikiwa ni ulipizaji kisasi kwa ukaliaji mabavu wa Israel wa miongo kadhaa.
Akiiunga mkono Israel, Biden alisema Marekani lazima pia iweke nia ya dhati kuisaidia Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Russia. “Historia imetufundisha kwamba magaidi hawalipi gharama kwa vitendo vyao vya kigaidi, wakati madikteta hawalipi gharama kubwa kwa uchokozi wao, wanasababisha vurugu zaidi na vifo na uharibifu mkubwa,” anasema Biden.
Biden hakusema anaomba kiasi gani – kiwango halisi kitajulikana leo wakati itakapowasilishwa kwenye Bunge.
Bunge lazima liwe na spika kupitisha hiyo sheria. Hadi hivi sasa, hakuna Mrepublican ameweza kupata kura 217 zinazohitajika ili kuchukua wadhifa wa spika, kufuatia kuondolewa kwa spika wa zamani Kevin McCarthy mapema mwezi huu.
Wakati huo huo, waandamanaji wanaotaka sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas walifika kwenye jengo la bunge la Capitol siku ya Jumatano. Ukusanyaji maoni uliofanywa na Reuters na Ipsos unaonyesha kuwa asilimia 41 wamesema Marekani ni vyema iunge mkono msimamo wa Israel. “Uongozi wa Marekani ndiyo unaoiweka dunia pamoja. Washirika wa Marekani ndiyo wanatufanya tuwe salama.”
Hoja itaangaziwa kwa mashaka. Malalamiko na nyakati nyingine ghasia, dhidi ya Israel na dhidi ya Marekani yamezuka katika miji mikuu mbali mbali kote duniani. Waandamanaji wengi wanaiona Israel kama mkaliaji wa kimabavu ambaye anaendelea kujiingiza katika maeneo ya Palestina, akiungwa mkono na Marekani hata wakati utawala unaposhutumu kujiingiza kwa Russia katika baadhi ya sehemu za Ukraine.
Forum