Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 alikamatwa kwa tishio la uongo la bomu nje ya Paris vyanzo vya polisi vilisema Ijumaa wakati mamlaka ya Ufaransa ikihangaika kusitisha wiki moja ya vitisho vya mabomu katika viwanja vya ndege, shule na maeneo ya kihistoria.
Msururu wa vitisho vya uongo vya mabomu umeikumba nchi hiyo ambayo iko katika tahadhari ya juu tangu shambulio la wanamgambo wa Hamas kwa Israel, vita vilivyoibuka huko Gaza na mauaji ya mwalimu mmoja kuchomwa kisu katika mji wa kaskazini wa Arras wiki iliyopita.
Kijana huyo alikamatwa Alhamis kufuatia tishio la bomu lililotumwa kwa barua pepe huko Saint-Ouen-I’Aumone mji ulio kaskazini-magharibi mwa Paris.
Takribani watu 1,200 wakiwemo angalau wanafunzi 1,000 waliondolewa katika shule ya msingi ya Jean Perrin mahala ambapo mshukiwa alikuwa anasoma huko.
Hakuna vilipuzi vilivyopatikana kufuatia uchunguzi katika eneo na azma kamili ya kijana huyo bado haijafahamika.
Forum