Kwenye hafla hiyo iliyofanyikia kwenye mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dessau, Scholz amesema kwamba utawala wake hautaruhusu kamwe maandamano dhidi ya wayahudi nchini mwake. “Ujerumani italinda maisha ya wayahudi,” amesema Scholz, wakati akieleza kushtushwa kwake na maandamano yanayoshuhudiwa kote ulimwenguni dhidi ya wayahudi, hata nchini mwake, tangu Oktoba 7 baada ya uvamizi wa Hamas dhidi ya Israel.
Nyumba za wayahudi mjini Berlin zimewekwa alama ya Daudi, wakati washambulizi mapema wiki iliyopita wakirusha makombora aina ya Motolov dhidi ya hekalu la kiyahudi mjini humo.
Forum