Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:12

Hamas yaachilia mateka wengine wa Israel


Hamas, Jumatatu iliachilia mateka zaidi ambapo wanawake wawili vikongwe wa Israeli, waliachiliwa wakati Israeli ikiimarisha mashambulizi yake ya anga Gaza.

Hayo yakiendelea Marekani, imeonyesha kuwa na wasiwasi kuhusu vita vya Israel na Hamas kwamba vinazidi kuwa vita vya mashariki ya kati.

Katika taarifa, Hamas, imesema iliwaachilia mateka hao kwa sababu za kibinadamu.

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilisema iliwasafirisha wanawake wa Israel, wenye umri wa miaka 85 na 79 kutoka Gaza Jumatatu jioni hadi Tel Aviv.

Kundi hilo la wanamgambo liliwaaachilia mateka wake wawili wa kwanza mama na bintiye wa Kimarekani, Ijumaa, ikiwa karibu ni wiki mbili baada ya kufanyika shambulizi la kushtukiza Israeli, na kuuwa zaidi ya watu 1,400, wengi wao wakiwa raia, na kuwakamata mateka zaidi ya 200 wengine.

Forum

XS
SM
MD
LG