Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:55

Israel yaendelea kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza Jumatatu


Picha ya eneo lililoharibiwa na makombora ya Israel huko Gaza. Kutoka maktaba.
Picha ya eneo lililoharibiwa na makombora ya Israel huko Gaza. Kutoka maktaba.

Jeshi la Israel Jumatatu limeendelea kufanya mashambulizi ya anga katika  Ukanda wa Gaza, wakati mawaziri wa mambo ya nje  kutoka Umoja wa Ulaya wakikutana kufikiria  sitisho la mapigano kwa misingi ya kibinadamu.

Ndege za Israel pia zimelenga maeneo kadhaa ya Hezbollah nchini Lebanon, yakiwemo maeneo ambayo jeshi limesema walikuwa wanajitayarisha kurusha makombora na roketi kuelekea Israel.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa EU Josep Borell amewaambia wanahabari kwamba anaamini sitisho la kibinadamu la mapigano linahitajika ili kuruhusu misaada kuwafikia watu wa Gaza.

Maoni yake yamekuja siku moja baada ya msafara wa pili wa malori ya misaada kuruhusiwa kuingia Gaza kupitia kivuko cha mpakani cha Rafah nchini Misri. Israel imefanya mashambulizi ya zaidi ya wiki mbili dhidi ya Gaza, yakiwa majibu ya shambulizi la Oktoba 7 kutoka kundi la wanamgambo la Hamas, ambapo watu 1,400 waliuwawa.

Viongozi wa Marekani,Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy na Uingereza, Jumapili wamezungumzia vita hivyo kwa njia ya simu kwa mwaliko wa rais wa Marekani Joe Biden.

Forum

XS
SM
MD
LG