Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 08:15

Israel yafanya mashambulizi zaidi Gaza


Israel ilifanya mashambulizi mapya makali ya anga ikilenga eneo linalo milikiwa na Hamas, Gaza kuelekea usiku wa Jumane, ambapo maafisa wa Palestina wanasema mamia ya watu waliuwawa ikijumuisha kambi ya wakimbizi.

Wakati ikiwa imesitisha kuanza mashambulizi ya ardhini kuingia ukanda ulozingirwa wa Palestina yakilenga kusambaratisha kundi la Hamas, jeshi la Israel linasema mashambulizi yake ya anga yamesambaratisha zaidi ya maeneo 400 katika kipindi cha saa 24 zilizopita baada ya kushambulia mengine 320 mapema mchana.

Wizara ya afya ya Gaza inayo shikiliwa na wanamgambo wa Hamas, imesema watu 704 wameuwawa, licha ya kwamba idadi hiyo haijaweza kuthibitishwa na chanzo huru.

Wizara ya afya ya Palestina Jumanne imesema kwamba vifo vya Gaza katika zaidi ya wiki mbili za mgogoro vinafikia 5,791.

Forum

XS
SM
MD
LG