Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 11:53

Mwito watolewa wa kusimamishwa mapigano Gaza


Mwito umezidi kutolewa Jumanne katika Umoja wa Mataifa wa kusimamisha mapigano baina ya Israel, na Hamas, kupisha hali ya kibinadamu.

Licha ya mwito huo inaonekana itakuwa ngumu kutekelezwa baada ya Hamas, kurusha roketi kwa Israel, ambapo pia Israel ilijibu kushambulia Hamas, katika ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Eli Cohen, ameueleza mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba itawezekana vipi kusimamisha mapigano na upande ambao umedhamiria kuua na kumaliza uwepo wako.

Ameitaka Qatar, ambayo ina uhusiano na Hamas, kuingilia ili kufanikisha zaidi kuachiliwa kwa raia wa Israel na wale wa kigeni 200 wanaoshikiliwa mateka.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Antony Blinken, amesema jumuiya ya kimataifa lazima ilishutumu kundi la Hamas, kwa shambulizi lake la kigaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG