Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:28

Vita vya Israel na Hamas vyatoa changamoto kwa azma ya mradi wa biashara inayounganisha India, Mashariki ya Kati na Ulaya



Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud, kushoto, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, katikati , na Rais wa Marekani Joe Biden wakihudhuria kikao cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Miundombinu na Uwekezaji wakati wa Mkutano wa G20 New Delhi, India, Sept. 9, 2023.
Prince wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud, kushoto, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, katikati , na Rais wa Marekani Joe Biden wakihudhuria kikao cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Miundombinu na Uwekezaji wakati wa Mkutano wa G20 New Delhi, India, Sept. 9, 2023.

Ghasia zinazoendelea kati ya Israel na Hamas zimedhihirisha changamoto zinazo kabili jitihada yenye azma ya kufungua njia mpya ya biashara kutoka India kupitia Mashariki ya Kati hadi Ulaya, hii ni kulingana na wachambuzi.

Ikitangazwa katika mkutano wa viongozi wa Kundi la G20 uliofanyika India mwezi uliopita, Njia ya Usafirishaji wa Kiuchumi kati ya India-Mashariki ya Kati – Ulaya au IMEC, inaonekana kama ni njia ya kisasa ya kusafirisha viungo na juhudi mbadala ya mradi wa China wa Belt and Road Initiative.

Mlango huo wa biashara unakusudia kuweka mtandao wa reli na usafiri wa baharini unaounganisha UAE, Saudi Arabia na Jordan hadi bandari ya Haifa ya Israeli katika bahari ya Mediterranean. Bidhaa zinaweza baadaye kusafirishwa hadi Ulaya, kwa kutopitia Mfereji wa Suez.

Lakini wakati Israel inafanya mashambulizi huko Gaza kujibu shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Hamas Oktoba 7, eneo hilo limetumbukia katika matatizo ya ukosefu wa usalama huku vita vikipamba moto na kuwa vibaya zaidi kuliko vita vitano vya Gaza vilivyotangulia.

“Hivi sasa tunakabiliwa na uwezekano wa kuenea kwa vita hivi katika eneo pana zaidi na hilo ni uthibitisho wa uhakika kwa IMEC,” kulingana na Chinatamani Mahapatra, muasisi wa taasisi ya Kalinga Institute of Indo Pacific Studies huko New Delhi. “Katikati ya mgogoro huu, mradi huu kamili wa IMEC unaelekea kutoweka.”

Forum

XS
SM
MD
LG