Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:04

Zambia yakubali mkataba wa Maelewano, MoU wa kurekebisha deni la dola biloni 6.3


Siku ya nne ya mkutano wa IMF na Benki ya Dunia mjini Marrakech, Morocco.
Siku ya nne ya mkutano wa IMF na Benki ya Dunia mjini Marrakech, Morocco.

Zambia imekubali kuingia katika mkataba wa maelewano (MoU) na wakopeshaji wake juu ya urekebishaji wa deni la takriban dola bilioni 6.3, karibu miaka mitatu baada ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kushindwa kulipa mkopo huo, wizara ya fedha ilisema Jumamosi.

Zambia ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kutolipa deni lake katika enzi ya janga la Corona na mchakato wake wa marekebisho umeipelekea kukubali masharti mapana ya kurekebisha deni hilo na wakopeshaji rasmi, wakiwemo China na wanachama wa Klabu cha Paris cha mataifa ya wakopeshaji mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Ijumaa, viongozi wa kifedha kutoka Kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20, walikaribisha kile walichokiita "mikakati iliyopiga hatua kubwa" kuelekea kukamilishwa kwa mkataba wa maelewano wa kushughulikia deni la Zambia na "hatua zinazoendelea" kuhusiana na deni la Ghana.

G20 pia ilitoa wito wa "kuhitimishwa haraka" kwa mazungumzo ya madeni yanayoendelea, ya Ethiopia na Sri Lanka, na kuhimiza juhudi za washiriki wa mazungumzo ya Madeni ya Kimataifa ili kuimarisha mawasiliano na kukuza maelewano ya pamoja kati ya wadau wakuu, ndani na nje ya Mfumo wa Pamoja wa G20 ili kuwezesha mipango ya msamaha wa deni.

Forum

XS
SM
MD
LG