Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:05

Rais wa Misri aonya kuwa vita vya Gaza huenda vikawa vya kikanda


Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi .
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi .

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi Jumamosi ameonya dhidi ya kuendelezwa kwa vita vya Gaza, akisema kwamba huenda vikahatarisha usalama wa kikanda.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiongozi huyo pia amesema kwamba utaifa wa nchi yake lazima uheshimiwe, baada ya drone kadhaa kunaswa Ijumaa baada ya kuingia kwenye anga ya Misri. Israel ilisema Ijumaa kwamba drone hizo zilikuwa zimeilenga, zikidaiwa kutumwa na wa Houthi wa Yemen, wanaoungwa mkono na Iran.

Jeshi la Misri limesema kwamba drone hizo zilianguka kwenye miji ya Taba na Nuweiba karibu na mpaka wa Israel, wakati zikijeruhi watu 6, zikitokea kwenye bahari ya Shamu, bila kutaja waliorusha. Sisi mapema Jumamosi ameitisha kikao cha kuruhusu misaada kuingia Gaza, kuachiliwa kwa mateka, pamoja na sitisho la mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG