Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:57

Biden apeleka ujumbe kwa Iran


Rais wa Marekani, Joe Biden, ametuma ujumbe wa nadra kwa kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, kutoa onyo kwa Tehran, kutolenga wanajeshi wa Marekani,  huko mashariki ya kati, imesema White House, Alhamisi baada ya mashambulizi kwa wanajeshi wa Marekani, katika kanda hiyo.

Msemaji wa White House, John Kirby, amesema katika mkutano na wanahabari kwamba kulikuwa na ujumbe wa moja kwa moja uliopelekwa licha ya kutofafanua ujumbe wenyewe.

Ubalozi wa Iran, katika Umoja wa Mataifa, haukujibu ulipoombwa kutoa maoni juu ya ujumbe wa Marekani, kwa kiongozi wa Iran. Maafisa wa Marekani, wanaepusha kufanya mgogoro kuwa mpana huko Mashariki ya Kati, kufuatia shambulizi la Oktoba, 7, la wanamgambo wa Hamas ambalo limeuwa watu 1,400 nchini Israel, wengi wao ni raia.

Takriban wanajeshi 900 zaidi wa Marekani, wanaelekea kwenye kanda hiyo, ama wameshawasili kuongeza ulinzi wa anga kulinda wanajeshi wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG