Sanaa na mikoa kadhaa ya kaskazini mwa Yemen iko chini ya udhibiti wa kikundi cha Wahouthi chenye mahusiano na Iran, ambacho kimekuwa katika vita tangu mwaka 2014 na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia yenye makao yake katika mji wa bandari wa Aden ulio upande wa kusini.
Mapigano yamepungua katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, ikileta unafuu kwa kile Umoja wa Mataifa ilichokieleza kuwa ni mgogoro mbaya kabisa wa kibinadamu duniani. Hata hivyo, mamilioni ya watu bado wanategemea misaada ya moja kwa moja ya kibinadamu.
WFP ilisema uamuzi huo ulichukuliwa kwa kushauriana na wafadhili na unakuja baada ya miaka kadhaa ya mashauriano na hakuna makubaliano yaliyofikiwa kupunguza idadi ya watu wanaopatiwa huduma hiyo kufikia milioni 6.5 kutoka milioni 9.5.
Akiba ya chakula katika maeneo yaliyo chini ya utawala wa Kihouthi inakaribia kumalizika na kuanzisha tena msaada wa chakula kuanzishwa tena unaweza kuchukua hadi miezi minne kutokana na kuyumba kwa usambazaji huo, Shirika la UN lilisema katika taarifa yake.
Hakuna maoni ya mara moja kutoka kwa maafisa wa Kihouthi.
WFP tayari ilikuwa imepunguza mgao nchini Yemen tangu mwaka 2022 kwa sababu ya uhaba wa fedha na mfumuko wa bei uliofuatia uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Shirika hilo lilisema litaendelea na programu nyingine, ikiwemo lishe na programu za kuzipatia shule chakula ili kupunguza athari za maamuzi hayo.
Usambazaji chakula kwa jumla utaendelea kujikita kwa wale wenye shida zaidi katika maeneo yanayo dhibitiwa na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia, ilisema.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum