Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:01

Idadi ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi duniani yafikia milioni 71.1


Alexandra Bilak
Alexandra Bilak

Idadi ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi kote duniani ilifikia rekodi ya milioni 71.1 mwishoni mwa mwaka 2022 , kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi na kituo kinachofuatilia idadi ya watu waliokoseshwa makazi.

Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 20 kuanzia mwaka 2021.

Miongoni mwa mambo yaliyochangia kukoseshwa makazi ni vita nchini Ukraine ambapo ripoti inasema kwamba ni watu milioni 17, na mafuriko makubwa yaliyotokea Pakistani yamewakosesha makazi watu milioni nane.

Duniani kote ghasia na mizozo inahusika kusabisha watu milioni 62. 5 kukosa makazi ndani ya nchi hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2022.

Takriban robo tatu ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi kote ulimwenguni wanatoka katika nchi kumi, miongoni mwa hizo ni DRC, Ethiopia, Somalia, Sudan, Nigeria na Yemen.

Alexandra Bilak Mkurugenzi wa Kituo cha Kufuatilia Watu Waliokoseshwa Makazi anasema: “ Kwahiyo ripoti kwa upande mmoja inaangalia idadi ya jumla ya watu ambao hivi sasa wamekoseshwa makazi ndani ya nchi hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana. Hii ina maanisha idadi iliyopo ni zaidi ya milioni 70 ya watu. lakini pia inaangalia rekodi ya idadi ya watu wanaohama ambazo zimerekodiwa kwa mwaka ili kutoa maana halisi ya hali za kukoseshwa makazi.

Bilak anaeleza zaidi: “ Kwa kuongezea, katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano iliyopita tumeona kwamba watu waliokoseshwa makazi kunatokana na mchanganyiko wa sababu mbalimbali. sio sababu moja inayopelekea watu kuondoka . haijawahi kuwa sababu moja tu kwa nini watu wanahama nyumba zao. Ni mchanganyiko wa sababu mbalimbali za kisiasa, kijamii, kiuchumi na mazingira ni moja wapo pia.

XS
SM
MD
LG