Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:03

Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan yafikia 700,000, Umoja wa mataifa wasema


Watu wanavuka mpaka wakitoroka mapigano nchini Sudan, waonekana kwenye kambi ya wakimbizi katika kauntu ya Renk, Sudan Kusini, Mei 3, 2023
Watu wanavuka mpaka wakitoroka mapigano nchini Sudan, waonekana kwenye kambi ya wakimbizi katika kauntu ya Renk, Sudan Kusini, Mei 3, 2023

Vita kati ya majenerali wa Sudan vinazidi kusababisha madhara mabaya kwa raia , huku idadi ya waliolazimishwa kuhama makazi yao ikiongezeka maradufu, Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne.

Mamia ya watu waliuawa kufikia sasa. Wasiwasi mpya umeibuka wakati mapigano tofauti ya kikabila yalisababisha vifo vya watu 16 kusini mwa nchi hiyo, na kundi lenye nguvu mashariki mwa nchi ambalo halijahusika katika vita, lilijitokeza na kuliunga mkono jeshi la taifa.

Zaidi ya watu 700,000 hivi sasa ni wakimbizi wa ndani waliohamishwa kwenye makazi yao kutokana na mapigano tangu Aprili 15, kulingana na shirika la kimataifa la uhamiaji.

“Jumanne wiki iliyopita, idadi ilikuwa 340,000,” msemaji wa Umoja wa Mataifa, Paul Dillon, alisema mjini Geneva.

Idadi kubwa ya watu wanavuka mipaka kutoroka mzozo kati ya wanajeshi watiifu kwa mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anaongoza kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).

XS
SM
MD
LG