Mazungumzi hayo ni ya kwanza kati ya serikali ya Syria na wawakilishi kutoka nchi za kiarabu tangu Syria ilipoondolewa kutoka muungano wa nchi za kiarabu mwaka 2011, kufuatia msako mkali wa utawala wa rais Bashar Al-Assad dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanapinga utawala wake.
Jordan imetaka Syria kufanya mazungumzo na nchi za kiarabu na kuweka mikakati ya kumaliza mapigano, kuwashughulikia wakimbizi, wafungwa, kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Mazungumzo pia yanaangazia wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran, walio nchini Syria.
Maswala hayo yote yanavuruga hali ya utulivu katika nchi Jirani na Syria.