Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:59

Marekani: Wanadiplomasia wawaambia wabunge wanamatumaini lakini kwa uangalifu kuhusu kufikiwa suluhu Sudan


Kamanda wa wanamgambo wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo (kulia) na Mkuu wa jeshi Abdel-Fattah Burhan
Kamanda wa wanamgambo wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo (kulia) na Mkuu wa jeshi Abdel-Fattah Burhan

Wanadiplomasia wa Marekani wamewaambia wabunge Jumatano kuwa wana matumaini lakini uangalifu kwamba pande zinazopigana nchini Sudan zitakubaliana juu ya sitisho la muda la mapigano kuruhusu misaada ya kibinadamu katika mazungumzo yanayofanyika Jeddah, Saudi Arabia.

Tangu katikati ya mwezi Aprili, watu 750 wameuawa katika mapigano na maelfu kukoseshwa makazi.

Sauti za milio ya risasi katika mitaa ya mji mkuu Khartoum zimeendelea kusikika hata wakati mashauriano ya amani kati ya kamanda Mohammed Hamdan Dagalo na mkuu wa jeshi Abdel-Fattah Burhan yanaonekana kuonyesha dalili nzuri katika mikutano inayofanyika Jeddah, Saudi Arabia.

Victoria Nuland, Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mausala ya Siasa ameeleza: “Kama hatua hii itakuwa na mafanikio, nimezungumzaz na wapatanishi wetu hivi asubuhi, ambao wana matumaini lakini uangalifu, basi itawezesha kupanua mazungumzo kwa wadau wengine katika eneo, kikanda na kimataifa kuelekea katika kupatikana kwa sitisho la kudumu la mapigano, na halafu kurejea kwenye utawala wa kiraia kama watu wa Sudan wamekuwa wakidai kwa miaka mingi.”

Victoria Nuland
Victoria Nuland

Burhan aliongoza mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021 – wabunge walisema kuwa Marekani imeshindwa kushughulikia hili.

Seneta Bob Menendez, Mwenyekiti Kamati Mambo ya Nje amesema: “Badala ya kuweka vikwazo, tunaweka utashi wa kidemokrasia wa mamilioni ya Wasudan, katika mikono ya majenerali, licha ya ushahidi kuhusu wanachokifanya na jukumu lao katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na rushwa kubwa ya umma.”

Sudan ilitakiwa kupitia kipindi cha mpito kuelekea serikali ya kidemokrasia. Mzozo umerudisha nyuma mpango huo – na baadhi ya wabunge warepublican wanasema utawala wa Biden bado haujandaa mkakati.

Seneta Jim Risch, Mrepublican anasema: “Nimeutaka utawala kuelezea mtizamo wa wazi kwa kile inachokita nchini Sudan. Bado nasubiri.”

Wiki iliyopita, White House iliidhinisha vikwazo ambavyo vinaweza kulengwa kwa mtu yeyote ambaye anadumaza uthabiti wa Sudan. Wabunge wengine walisema kuwa kuendelea kwa mashauriano ya amani yana lengo la wazi kabisa.

Seneta Chris Van Hollen, Mdemocrat amesema: “Tunataka kuona sitisho la mapigano. Tunataka kuona linadumu, kutoa muda kwa mashauriano. Lengo linalotakiwa, kwa kweli, ni kuirejesha Sudan kwenye njia ya kuelekea katika demokrasia ambako watu wa Sudan wanasema kuwa na sauti.”

Zaidi ya theluthi moja ya watu nchini Sudan walikuwa wakihitaji misaada ya kibinadamu kabla ya mzozo kuanza, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan – na hivi sasa hali ni mbaya sana.

Wakimbizi wa Sudan wakiwa nchini Chad May 9, 2023. REUTERS/Zohra Bensemra
Wakimbizi wa Sudan wakiwa nchini Chad May 9, 2023. REUTERS/Zohra Bensemra

Sarah Charles, USAID Kitengo cha Misaada ya Kibinadamu amesema: “Zaidi ya watu laki saba wamekoseshwa makazi ndani ya nchi, na zaidi ya laki moja na elfu sabini wamevuka na kuingia katika nchi jirani, ikimaanisha kuwa athari za mzozo haiishii tu katika mipaka ya Sudan. Zinaingia katika kanda nzima, na kusababisha mkanganyiko katika mahitaji ya kibinadamu kote katika nchini kadhaa.”

Maafisa wa wizara ya mambo ya nje wamewaambia wabunge kuwa wamefanikiwa kuwaondoa wamarekani 1,300 kati ya 5,000 waliojiandikisha nchini Sudan – hao waliobakia wakiamua kubaki nchini humo.

XS
SM
MD
LG