Wakati bandari imekuwa ndiyo njia kubwa kupitia Sudan magari makubwa yaliyosimama yaliashiria kuwa mzozo mkubwa unakuja.
Pande mbili zinazogombana nchini Sudan zilianza mazungumzo Jumamosi yenye lengo la kuimarisha sitisho la mapigano lililoshindwa baada ya wiki tatu za mapigano ambayo yameuwa mamia ya watu.
Taarifa chache zimetolewa kwa umma kuhusu mazungumzo hayo yanayoongozwa na Saudi Arabia na Marekani mjini Jeddah kati ya jeshi la Sudan SAF na kikosi cha RSF yaliyoanza Mei 6.
Lakini kiongozi wa SAF Jenerali Abdel Fattah al Burhan Jumatatu alikiambia kituo cha televisheni cha Misri βAl-Qahera News TV, kwamba hakuna umuhimu wa kuketi pamoja kwenye meza ya mashauriano nchini Saudi Arabia bila ya kuwa na sitisho la mapigano la kweli.
Jenerali Burhan amesema anakaribisha juhudi zote zenye lengo la kusitisha umwagaji damu lakini akasisitiza kwamba RSF lazima iweke silaha zake chini.