Wajumbe kutoka pande mbili zinazohasimiana nchini Sudan wako Saudi Arabia kupanga kufunguliwa kwa njia za kibinadamu nchini Sudan.
Pande hizi zimesisitiza kwamba zimekutana ili kila mmoja alete afueni kwa hali ya kibinadamu katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na sio kuhusu mashuariano ya sitisho la mapigano.
Mashauriano ya mwanzo yalianza Jumamosi. Ufalme wa Saudi Arabia tayari umeahidi kuipatia Sudan misaada ya kibinadamu ya thamani ya dola milioni 100. Mapigano yalizuka nchini Sudan kati-kati ya April. Baada ya wiki kadhaa za mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na kikosi cha RSF, maelfu ya wa-Sudan wamelazimika kukimbia makazi yao huku wasudan waliokoseshwa makaazi Sudan wakitafuta hifadhi katika nchi zinazopakana nazo.
Pande hizo mbili, jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel-Fattah Burhan na kikosi cha Rapid Support Forces kinachoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, hawajakutana tangu mapigano yalipozuka hapo April 15.