WHO imesema Jumanne kwamba zaidi ya watu 5, 000 wamejeruhiwa kutokana na mapigano hayo baina ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF.
Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yameshindwa kumaliza mzozo au hata kufanya ili kupunguza ghasia .
Umoja wa Mataifa umesema mlipuko wa mapigano Sudan unataabisha hali ya kibinadamu Abyei katika mpaka wa Sudan Kusini na Sudan.
Hanna Serwaa Tetteh , mwakilishi wa umoja wa mataifa katika umoja wa Afrika anaeleza: “Wakati mamlaka za Sudan hivi sasa haziko katika nafasi ya kulinda mipaka yake hali ya ukosefu wa usalama mpakani baina yaSsudan na Sudan Kusini inaweza kuongezeka wakati wa harakati za kuvuka mpaka kwa makundi yenye silaha na ya uhalifu."
Ameongeza kuwa: "Mapigano nchini Ssudan pia yanaathiri shughuli za kibiashara za kila siku na usambazaji wa chakula na bidhaa nyingine muhimu kutoka Sudan kwenda Sudan Kusini na kuhatarisha uuzaji wa mafuta kutoka kusini.”
Wajumbe wa pande zote mbili wamekuwa wakikutana mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa siku kadhaa kwa lengo la kufikia makubaliano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya watu wenye shida ya chakula, makazi, huduma za afya mjini Khartoum na miji mingine ya Sudan.
Saudia Arabia tayari imeahidi kwamba itaipa Sudan misaada yenye thamani ya dola milioni 100.