Hali hiyo pia huenda ikaongeza ujasiri wa mataifa mengine yenye nia kama hiyo, kote ulimwenguni aliongeza Stoltenberg. Wakati akifanya mahojiano na televisheni ya Fox News Sunday, Stoltenberg pia alisema kwamba Beijing inafuatilia kwa karibu, hatua za NATO kuhusu uvamizi wa Putin wa Ukraine.
βLeo ni Ukraine, na kesho huenda ikawa Taiwan,β aliongeza Stoltenburg. Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba kupungua kwa misaada kutoka Marekani kwa Kyiv huenda kukatuma ujumbe potofu, kwa kuwa rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akizuiliwa kuidhinisha msaada zaidi na warepablikan waliopo kwenye Baraza la wawakilishi.
Wakati msaada wa Marekani ukionekana kushuka, Zelenskyy ameomba Ujerumani itumie uwezo wake wa kifedha kurai washirika wengine wa EU, kuongeza msaada wa Kyiv, inapoendelea kukabiliana uvamizi wa Russia.
Forum